A Closer Walk
Encourage One Another Daily - As Long As It Is Called Today! (Hebrews 3:13)

Home Today Archive Salvation About Resources Add Name
Reading Plans | Verses | Forums | Support | Spanish Devotionals
Book Store  |  Translations  Africa Ministry  |  Stacey Blog | Podcast | NEW!! Facebook !!!

 


A Closer Walk - Volume 1 Archive

English Message | Spanish Message

Mpe Yeye Utukufu Wote

Yusufu alikumbwa na wakati mgumu katika miaka yake ya mwanzo. Ndugu zake walijaribu kumuua lakini wakamwuza kwa wamidiani wamidiani, nao walikuwa kama mtumwa kwa potifa aliyekuwa mmojawao wa akida wa Farao. Yusufu hatimaye alizingiziwa na mke wa Potifa na akatupwa gereezani alikokaa kwa miaka kadhaa - mambo bila shaka hayakuwa yakienda vizuri.
Halafu siku moja Yusufu alipata fursa kufanya mabadiliko. Farao aliota ndoto ambazo zilimfadhaisha sana. Lakini aliwaita watu wote wenye hekima wa misri, hukuna aliyeweza kumfasiria, “Farao akwahadithia ndoto yake, wala hakuna aliyeweza kumfasiria farao mambo hayo” (Mwanzo 41:8). Farao aliambiwa palikuwa na kijana Mwebrania, mtumishi aliyekuwa gerezani, ambaye alikuwa amedhihirisha uwezo kufasiri ndoto.
Farao kwa haraka alimwita Yusufu kutaoka gerezani; “nami nimeskia habari zako, ya kwamba, usikiapo ndoto, waweza kuifasiri” (Mwanzo 41:15). Wau! Hii ilikuwa nafasi kubwa ya Yususfu – Fursa yake ya kuchukuwa mambo mikononi mwake na kutengeneza hatima yake. Kakika alistahili pumziko. Hata hivyo, si Mungu huwasaidia wanaojisaidia?
Kwa bahati mbaya, hii ni mojawapo ya kasoro za kuinukuu Biblia – na aibu ya kumudhirisha Mungu. Ni sahihi kabisa kusema Mungu kwa uaminifu atafanya hatima yetu kuwa nzuri tunapomtafuta Yeye kwa dhati na kumpenda Yeye kwa moyo wetu wote; na kwa uaminifu kufuata anakotulekeza Yeye.
Yusufu angeweza kutumia fursa hii kujiletea utukufu na heshima. Lakini alikuwa amejifunza funzo mihimu kuwa vitu VYOTE vinatoka kwa Mungu na vinapaswa kutumiwa kwa utukufu wa Jina Lake.
Mwanzo 41:16
“ Si mimi, Yusufu akamjibu Farao, Mungu atampa Farao majibu ya amani”
Yusufu alikuwa amepewa kipawa cha ajabu, lakini kipawa hiki kiliweza tu kuzaa kupitia maisha ya Yusufu. Hii lilikuwa funzo sawa na ile alilofundisha kanisa la Wakorinthio: “Nawe una nini usichokipokea? Lakini iwapo ulipokea wajisifia nini kana kwamba hukupokea” (1Wakorithio 4:7).
Ni kwa neema ya Mungu tunafanyea lolote; “maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.” (Yohana 15:5). Ni kwa neema yake tuna vipawa na uwezo – ni kwa neema yake tumepata muelekeo na motisia. Hikika, kwa neema yake tunapumua mara nyingine! Kama Mungu anatupa vyombo vyote, hakika anastahili sifa ZOTE. Wacha tusikose fursa ya kutumia vipawa tulivyopewa na Mungu Na Maisha yetu yanapozaa matunda, tusikose fursa ya kumpa Yeye utukufu wote!
Kuwa Na Siku Njema!
Steve Troxel
God's Daily Word Ministries