A Closer Walk
Encourage One Another Daily - As Long As It Is Called Today! (Hebrews 3:13)

Home Today Archive Salvation About Resources Add Name
Reading Plans | Verses | Forums | Support | Spanish Devotionals
Book Store  |  Translations  Africa Ministry  |  Stacey Blog | Podcast | NEW!! Facebook !!!

 


A Closer Walk - Volume 1 Archive

English Message | Spanish Message

Jiunge Vitani

Kwenye ujumbe “Tutashinda” tulihimizwa kushikilia Yesu nguvu yetu inapodidimia na kudhofika. Tuliona kwamba kuendeleza imani yetu (sio nguvu yetu) huhakikisha tumeshinda na kupokea taji la uzima wa milele. Tunaweza kuchukuwa faraja kubwa tukijua Yesu atatubeba ba hatatuacha tuanguke, lakini lazima pia tukumbuke kuwa hatukuzaliwa katika familia yake ili tubebwe daima: “Bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya. Watapanda juu kwa mbawa kama tai” (Isaya 40:31). Tunapomkarimbia Mungu kupitia wakati mtulivu uliotengwa kwa mombi, atatupa nguvu mpya; na anapofanya, lazima tena twende vitani.
Mara kwa mara tunashau kuna vita vinapiganwa karibu nasi. Hatukui wasikivu kwa sababu hatuoni kweli vita. Hakuna matangazo rasmi ya nguvu za adaui na habari zinazoangazia majeruhi. Lakini usikosee … ni vita!
Waefeso 6:12
“Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majesi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.”
Kama vile hakika kulivyo na Mungu aliyemtoa mwana wake afe kwa ajili ya dhambi zetu, kuna pia Ibilisi na majesi ya peopoe wabaya wakifanya vita. Habari njema ni kwamba tunajua matokeo ya mwisho ya vita hivi; “Na yule Ibilisi, mwenye kuwandanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti“ (Ufunuo 20:10).
Hatima ya ibilisi ni dhahiri; lakini kwa sasa, yu katika njama ya kuwanaza wengi awezavyo; “Na iwapo mtu ye yote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto” (Ufunuo 20:15). kiwango cha vita hivi ni cha juu. Adui anaendelea kushambulia na kufurahi tunapofikiria tumeshindwa.
Lakini hatujasindwa! Tunaweza kupoteza mtazamo wetu; tunaweza kuyamba kutoka kwa lililo bora na kutumaini kwa vitu ambavyo vinafifia; tunaweza hata kukumbwa na wakati wa hofu na shaka; lakini hatujashindwa kwamwe! Barabara ya ushindi imewekwa miguuni petu. Inaanza kwa hatua yetu nyingine ya ushupavu ya kujongea karibu na Mungu na kumpenda Yeye kwa moyo wetu wote.
Nguvu yetu inaporejea (naitarejea!) lazima tuchukue Neno la Mungu na tuwe askari! Kuna wengi karibu nasi wenye vidonda vikubwa ambao “Wanakufa” kwa msaada. Tusiridhike kuketi kando au kubebwa daima. Wacha tukatoe maisha yetu kwa Mungu na tumuruhusu yeye afanye kazi kupitia kwetu kuwahimiza wengine kwa matembezi yao na kushiriki fahari ya Yesu na yeyote anayevuka njia yetu. Wacha tukatenge maisha yetu tena kwa imani isiyozimwa na, mara nyingine, jiunge vitani.
Kuwa Na Siku Njema!
Steve Troxel
God's Daily Word Ministries